Aina za jamhuri duniani
*Nyekundu - Serikali ya kiraisi
*Kijani - Serikali ya raisi pamoja na athira kubwa ya bunge
*Kijani-kizeituni - Serikali ya kiraisi pamoja na waziri mkuu
*Machungwa - Serikali ya kibunge
*Kahawiya - Jamhuri zinazoruhusu chama kimoja pekee
Mengine: Ufalme au serikali ya kijeshi
Angalizi nchi mbalimbali zinazojiita "jamhuri" hutazamiwa na wengine kama udikteta. Ramani ianonyesha hali ya kisheria si hali halisi.

Serikali ya kiraisi ni muundo wa siasa ambako serikali imo mikononi mwa rais wa nchi. Rais huyu anaunganisha nafasi za Mkuu wa Dola na pia kiongozi wa serikali.

Muundo huu ni tofauti na serikali ya kibunge ambako rais ni zaidi cheo cha heshima tofauti na kiongozi wa serikali ambaye huchaguliwa na bunge lenye madaraka ya kumwondoa tena.

Tabia za serikali ya kirais

Tabia za utaratibu huu mara nyingi ni:

Mifano

Faida na hasara

Kati ya faida za utaratibu wa kirais hutajwa mara nyingi serikali imara yenye nguvu katika utendaji. Kiongozi wa taifa ana nafasi kubwa kufuata siasa anayoiona ni lazima kwa mema ya nchi, hata kama wabunge wameanza kusitasita au kuogopa hasira ya wananchi. Kazi ya serikali inategemea nia ya mtu mmoja aliyepewa na wananchi wote nafasi na muda wake. Anayeangaliwa ni haki yake na pia wajibu wake kutumia madaraka haya.

Nguvu hii ni pia udhaifu wa muundo huo: kama rais ni mtu hafifu au mtu anayekosa uelewano mwema wa matatizo yaliyopo. Pia madaraka makubwa ya rais yameonekana kurahisisha kuundwa kwa udikteta kama huyu rais akitumia madaraka yake kubadilisha mgawanyo wa madaraka kati ya matawi ya dola yaani serikali, bunge na mahakama.

Muundo wa kumbakumba ya Serikali

Nchi mbalimbali hutumia utaratibu wa kuunganisha tabia za serikali ya kirais na serikali ya kibunge. Mfano wake ni Ufaransa ambako rais anayechaguliwa na wananchi wote hushirikiana na waziri mkuu anayetegemea bunge. Rais ana madaraka kadhaa pamoja na haki ya kuongoza mikutano ya mawaziri akitaka. Ana haki ya kutoa mwongozo juu ya siasa ya nje na pia ni mkuu wa jeshi.

Lakini anahitaji kushiriki katika kempeni za bunge na kuomba wananchi kumpa wabunge watakaoshikamana naye. Kama wananchi wanaamua tofauti anapaswa kushirikiana na waziri mkuu asiyekubaliana naye katika siasa. Hii ni njia mojawapo ya kuwapa wananchi nafasi ya kuweka mipaka kwa madaraka na uwezo wa rais wakiona asiamue kila kitu tena pekee yake.