Jiwe la Rosetta kutoka Misri ya Kale ni kati ya mifano ya kwanza ya tafsiri (ina matini ileile kwa lugha tatu).

Tafsiri (Asili ya neno hili ni Kiarabu; kisawe cha neno hili ni Tarjuma) ni kazi ya kutoa maana ya maneno kutoka lugha moja kwenda lugha nyingine.

Mtu anayefanya kazi hii huitwa mfasiri au mkalimani.

Kutafsiri na kukalimani kuna maana mbili kwa mujibu wa Kamusi Kuu ya Kiswahili (KKK):

  1. Ni kutoa andiko au maelezo fulani katika lugha nyingine kwa maana ilele.
  2. Toa maelezo ya lugha fulani kwa lugha nyingine kwa maana ileile kwa kutumia maandishi. Katika maana ya pili, maana yake ni kitenzi elekezi, ni kitenzi ambacho kinapokea Yambwa, yaani nomino ya mtendwa.

Katika misingi ya kielimu dhana ya tafsiri imeweza kujadiliwa na wataalamu mbalimbali.

Aina za matini

Kuna aina kuu mbili za matini, ambazo ni:

  1. Matini chanzi/ Chasili (Source text): Ni matini ambayo iko katika lugha yake ya awali au lugha yake iliyoandikiwa kabla ya mchakato wa kutafsiri.
  2. Matini lengwa/ Tafsiri (Target text): Ni matini iliyotafsiriwa kutoka lugha yake iliyoandikiwa.

Kumbuka:

  1. Lugha Chanzi/Chasili (LC) ni lugha iliyotumika kuandikia matini chanzi (Source language)
  2. Lugha Lengwa (LL) (Target language) ni lugha iliyotumika kutafsiria matini chanzi au lugha unayoitumia kufanyia tafsiri.

Ugumu wa kutafsiri

Hakuna tafsiri kamili kabisa. Kila mfasiri hana budi kuchagua kati ya mawili:

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Tafsiri
Makala hii kuhusu mambo ya fasihi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tafsiri kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.