Peni ya zamani.

Uandishi ni njia ya mawasiliano kati ya watu inayowakilisha lugha na hisia kwa alama na ishara zilizorekodiwa.

Katika lugha nyingi, uandishi unakamilisha mawasiliano ya sauti, ukitumia miundo yake, kama vile maneno, sarufi na semantiki.

Uandishi si lugha ya pekee, bali aina ya teknolojia iliyostawi pamoja na vifaa wilivyotengenezwa katika jamii fulani.

Kilichopatikana kwa njia ya uandishi kinaitwa matini, na anayeyapokea anaitwa msomaji.

Sababu za kuandika zinajumuisha barua, hadithi, shajara na kutoa vitabu.

Uandishi umewezesha kutunza kumbukumbu za historia, kudumisha utamaduni, kusambaza ujuzi na kuunda mifumo ya sheria.

Pia ni muhimu katika kumwezesha mtu kutokeza ya kwake, kama wanavyofanya washairi na watunzi wengine.

Kadiri jamii zilivyostawi, zilihitaji mabadilishano ya taarifa, utunzaji wa kumbukumbu mbalimbali (k.mf. hesabu, sheria na mikataba).

Kufikia milenia ya 4 KK, biashara na utawala huko Mesopotamia vilizidi uwezo wa kumbukumbu ya binadamu na kuhitaji maandishi;[1] vilevile katika Misri ya Kale na Amerika ya Kati.

Tanbihi

  1. Robinson, 2003, p. 36

Marejeo

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Uandishi

Viungo vya nje