Maabadi ya Wamandayo huko Nasiriya, Iraq.

Ujuzilio (pia: Unostiki, Gnosi; kwa Kiingereza: "Gnosticism", kutoka neno la Kigiriki γνωστικός, gnostikos, "mwenye ujuzi", ambalo mzizi wake ni γνῶσις, gnōsis, "ujuzi") ni nadharia ya wokovu kupatikana kwa njia ya maarifa.pia

Historia

Mazingira ya asili ni Uyahudi wa karne ya 1 na ya 2 BK.

Wafuasi wa Gnosi hiyo, wakitafsiri namna yao Torati na vitabu vingine vya Biblia, walidai ulimwengu unaoonekana haukuumbwa na Mwenyezi Mungu, bali na roho nyingine iliyofunga chembe ya Umungu katika mwili. Walidai kuwa maarifa, si imani, yanaweza kukomboa hiyo chembe.

Nadharia hiyo ilistawi hasa kando ya Bahari ya Kati, ikichanganyikana na falsafa ya Plato na matapo ya Ukristo yaliyopingwa na uongozi wa Kanisa kama uzushi.

Kuanzia karne ya 3 nguvu ya nadharia hiyo ilipungua, lakini bila kufutika kabisa katika ustaarabu wa magharibi hadi leo. Kwa mfano, ulijitokeza katika Renaissance.

Dini maalumu iliyoanzishwa kwenye msingi wa unostiki ilikuwa Umani (Manichaeism). Kutoka Dola la Persia, unostiki huo ulienea hadi China.

Leo hii kuna jumuiya moja iliyotokana na unostiki wa kale ambayo ni jumuiya ndogo ya Wamandayo katika Iraki na kusini mwa Iran.

Vyanzo

Vitabu

Tovuti

Marejeo mengine

Vyanzo vikuu
Vya jumla
Wasethi

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Ujuzilio
Texts
Encyclopedia
Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.