Mifano |
---|
|
Kivumishi ni neno/maneno yanayotoa taarifa ya ziada katika nomino. Kivumishi hufanya kazi ya kufafanua/kuelezea zaidi kuhusu nomino ili kupambanua/kuitofautisha nomino husika miongoni mwa nomino nyingine.
Kiwakilishi ni aina ya maneno ambayo husimama kuwakilisha nomino. Kivumishi hutoa taarifa ya ziada kuhusu nomino, kiwakilishi (endapo nomino haipo) au kivumishi chenzake (endapo kuna vivumishi zaidi ya kimoja katika tungo husika).
Inafanana kabisa na orodha ya viwakilishi, tofauti yake ni hali ya nafsi tu. Yaani, hakuna kivumishi cha nafsi.
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Vivumishi kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |