Lake Magadi
Mahali Bonde la Ufa
Anwani ya kijiografia 1°52′S 36°16′E / 1.867°S 36.267°E / -1.867; 36.267
Nchi za beseni Kenya
Eneo la maji 100 km²

Ziwa Magadi lipo kusini mwa Kenya katika eneo la Bonde la Ufa, kaskazini mashariki kwa Ziwa Eyasi.

Ni ziwa la chumvi na kiwango chake cha uchumvi kinazidi asilimia 30[1]. Limepokea jina lake kutokana kiasi kikubwa cha magadi (kabonati ya sodiamu) ndani ya maji yake; wakati wa kiangazi maji ya ziwa hupungua na % 80 ya eneo lake hufunikwa na chumvi hii. Wakati wa msimu wa mvua chumvi huwa inafunikwa tena kwa maji, kisha uzidi tena maji yanapokauka na kuacha chumvi nyeupe.

Ni maarufu kwa aina mbalimbali za ndege wanaoishi kandokando ya ziwa hilo, kwa mfano flamingo.

Ziwa Magadi lina ukubwa wa kilomita mraba 100 na huwa limejaa maji iliyokolea kabonati ya sodiamu ambayo huwa na kiasi kikubwa cha madini ya trona. Asili ya chumvi hii ni chemchemi moto zinazopatikana katika bonde la Ufa. Chemchemi hizo huwa kaskazini magharibi na kusini mwa ziwa hili.

Kuna aina moja tu ya samaki kwenye ziwa hili: cichlid Alcolapia grahami. Samaki huyu anaishi kwenye chemchemi moto zilizo kwenye ufukwe wa ziwa hili.

Ziwa Magadi hapo awali halikuwa na kiwango kikubwa cha chumvi. Miaka elfu kadhaa iliyopita (kipindi cha Pleistocene) na katikati ya kipindi cha Holocene lilikuwa na samaki wengi na kiwango cha chumvi kilikuwa cha chini. Kuna muda wa kihistoria ambamo Ziwa Magadi na Ziwa Natron yalikuwa yameshikamana kuwa ziwa moja kubwa.

Ziwa Magadi kutoka anga za mbali.

Mji wa Magadi upo kwenye pwani ya mashariki ya ziwa hili. Kiwanda cha soda Magadi kinapatikana kwenye mji huu.

Visiwa vinavyopatikana katika Ziwa Magadi

Tazama pia

Tanbihi

  1. Susanne Baumgarte: Microbial Diversity of Soda Lake Habitats (2003), tasnifu ya umahiri, Chuo Kikuu cha Braunschweig / Ujerumani

Marejeo