Gaziantep (kwa Kiosmani Kituruki; Ayintap; jina la zamani na hadi leo linatumika kufupisha kama: Antep) ni mji mkuu wa Jimbo la Gaziantep nchini Uturuki. Mji huu unatazamwa kama moja kati ya miji ya kale duniani ambayo hadi leo bado inakaliwa.
Mji huo una vituo viwili vya utawala wa wilaya zake, Şahinbey na Şehitkamil, na unakaliwa na wakazi wapatao 1,237,874[1] (2007) na una eneo la kilomita za mraba zipatazo 2,138.[2]
Huu ni mji wa sita kwa ukubwa nchini Uturuki na ndio mji mkubwa katika Anatolia ya Kusini-Mashariki - Uturuki.
Mji ulikuwa ukijulikana na Wagiriki wa Kale na Waroma kama Doliche au Dolichenus (kwa Kituruki: Dülük). Waarabu, Waseljuk, Waosma walilijua kama ʿAintab au Aïntab, ambalo linatokana na Kiarabu Ayn (chemchem) na tab (nzuri).
Tangu tarehe 8 Februari 1921,[3].
Mji ulipewa jina rasmi la Gaziantep, gazi kwa Kiarabu likiwa na maana ya mkongwe.
Makala hii kuhusu maeneo ya Uturuki bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Gaziantep kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |