Koti (kutoka Kiingereza: coat)) ni vazi linalovaliwa na jinsia yoyote kwa minajili ya kupata joto na pia kwa uanamitindo (fasheni).
Koti huwa na mikono mirefu (long sleeve) na huwa wazi kwa upande wa mbele ambapo waweza kufunga kwa kutumia vifungo, mnyororo au mshipi. Koti pia huenda ikawa na kofia au hoodie ya kuvalia kichwani.
Kamusi ya Kiingereza ya Oxford ina ithibati kwamba vazi hilo lilianza kuvaliwa tangu karne ya 13 ambapo jina coat lilikuwa likiandikwa kama cote. Jina coat linatokana na lugha ya Kifaransa na Kiitalia.
Katika Karne za Kati na renaissance, koti lilikuwa na urefu wa wastani, lenye vifungo kwa upande wa mbele na lenye skati yake iliyokuwa lazima iambatane na koti lenyewe. Hivi leo, hili halipo.
Hivi leo, kuna koti aina nyingi, kama vile:
![]() |
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Koti kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |