Mtindo wa Mozaiki ya Kiarabu katika kanisa kuu la Monreale, Sisilia, Italia, karne ya 12).
Mozaiki ya mawe mweupe na meusi kwenye sakafu ya nyumba ya Ugiriki ya Kale
Nakshi ya mawe katika sakafu ya ikulu ya Shapur I huko Bishapur.
Nakshi huko Uruk, Mesopotamia Milenia ya 3 KK.
Nakshi ya Kaisari Fransisko Yosefu wa Austria.
Nakshi ya Ugiriki wa Kale huko Pella, karne ya 4 KK, Pella Archaeological Museum.
Nakshi ya Kiroma huko Kartago. Iko katika Bardo Museum, Tunisia.
Nakshi ya Kiroma aina ya Cave canem ('Jihadhari na mbwa').
Sehemu ya The Great Pavement, nakshi ya Kiroma ya mwaka 325 huko Woodchester, Gloucestershire, Uingereza.
Kapteni wa Kigoti, kutoka ikulu ya Konstantinopoli, Uturuki.
Mtume Petro katika Chora Church.
Mtakatifu Demetrio katika Basilika lake huko Thessalonike.
Kristo Pantocrator katika Hagia Sophia, Konstantinopoli.
Theodoro Metochites akitoa Chora Church kwa Kristo.
Nakshi katika Santa Maria Maggiore, Roma, Italia.
Batizio ya Firenze.
Nakshi katika Basilika la Mt. Petro, Vatikano.
Yerusalemu katika nakshi maarufu kama Madaba Map.
Kugeuka sura kwa Yesu katika monasteri ya Mt. Katerina, Mlima Sinai, Misri.
Sehemu ya nakshi ya sakafuni katika kanisa la Masada.
Sehemu ya nakshi ya sakafuni katika kanisa la Petra.
Nakshi ya karne ya 12 huko Kiev, Ukraina, inayomuonyesha Mt. Demetrio.
Sehemu ya nakshi ya sakafuni katika sinagogi la Sepphoris
Nakshi ya dhahabu katika kuba ya Mskiti mkuu wa Cordoba, Hispania (965-970).
Mbinu mojawapo ya kutengeneza nakshi Li Jiang, Yunnan, China.
Wasanii wa nakshi wakipamba kanisa la Sagrada Família, Barcelona, Hispania.

Mozaiki (au mosaiki) ni mtindo wa pekee wa uchoraji picha unaotumia vipande vidogo vya kioo cha rangi au vijiwe au vigae vya rangi mbalimbali vinavyounganishwa kuwa picha. Kunawezekana pia kutumia vipande vya vitu vyovyote vyenye rangi vinavyoweza kuunganishwa kuwa picha.

Chanzo cha mtindo wa mozaiki

Mtindo huu ulionekana mara ya kwanza huko Phrygia (katika Uturuki ya leo) iliyokuwa sehemu ya ustaarabu wa Ugiriki ya Kale. Mawe ya rangi nyeupe na nyeusi yalipangwa ukutani au kwenye sakafu kuwa tarakibu.

Kichwa cha mungu Amfitriti kutoka nyumba ya Herkulaneo ya karne ya 1 KK.

Baadaye Wagiriki na zaidi Waroma waliendelea kuongeza rangi na kutunga picha kamili si tarakibu tu kwenye kuta za nyumba. Maghofu ya Kiroma yanaonyesha mifano mingi iliyodumu hadi leo.

Mozaiki za Bizanti na za Waarabu

Sanaa ya mozaiki iliendelezwa katika ustaarabu wa Bizanti. Wabizanti walipamba makanisa, majumba ya kifalme na pia nyumba za matajiri kwa mozaiki nzuri kabisa.

Waarabu Waislamu walipotwaa shemu kubwa za milki ya Bizanti waliendelea kuwaajiri wasanii Wabizanti wakipamba misikiti kama msikiti wa Umawiya huko Dameski au majumba ya masultani.

Baadaye walikuwa mafundi Waislamu waliopamba makanisa na nyumba katika Italia ya kusini.

Mozaiki leo

Mtindo wa mozaiki umeaendelea kutumiwa hadi leo. Kwa kawaida mozaiki inaendelea kuwa picha inayounganishwa kwa njia ya kudumu na ukuta au safau ya jengo fulani. Inawezekana pia kuifunga katika fremu na kubadilisha mahali pake lakini picha za mozaiki huwa nzito.


Mifano ya mozaiki

Tanbihi

Vitabu vingine

Viungo vya Nje

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Mosaic (Roman)


Makala hiyo kuhusu "Mozaiki" inatumia neno ambalo si kawaida na matumizi yake ni jaribio kwa jambo linalotajwa.
Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao.

Kamusi za Kiswahili ama zinatofautiana kuhusu matumizi ya neno hili au hazieleweki au hazina neno kwa jambo linalojadiliwa.

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Category:Mosaics