Logo for University of Dar es Salaam
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Mlimani
Wito kwa KiswahiliHekima ni Uhuru
Kimeanzishwa1961
AinaChuo cha Umma
WakfuChuo cha kwanza Tanzania
ChanselaDkt. Jakaya Mrisho Kikwete
Makamu wa chanselaProf. William A.L. Anangisye
DeanMs. Paulina Mabuga
MahaliDar es Salaam, Tanzania
KampasiMain Kampasi, CoICT Kampasi, DUCE Kampasi, MUCE Kampasi, Zanzibar Kampasi, SJMC Kampasi na Mbeya Kampasi
RangiBluu, Nyeupe
MsimboMlimani, UDSM
Tovutihttps://www.udsm.ac.tz/
Hekima ni Uhuru
Ukumbi wa Nkrumah.

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (CKD) (kiingereza: University of Dar es Salaam) ni chuo kikuu cha kwanza nchini Tanzania[1] chenye kauli mbinu inayosema Hekima ni Uhuru. CKD kina kampasi mbalimbali kama vile Main Kampasi, CoICT Kampasi, DUCE Kampasi, MUCE Kampasi, Zanzibar Kampasi, SJMC Kampasi na Mbeya Kampasi. Hizi Kampasi zipo mahali mbalimbali. Main Kampasi, CoICT Kampasi, DUCE Kampasi na SJMC Kampasi zinapatikana jijini Dar es Salaam. MUCE Kampasi inapatikana mkoa wa Iringa. Zanzibar Kampasi inapatikana Zanzibar. Mbeya Kampasi inapatikana jijini Mbeya.

Historia yake

Kiwango cha Elimu

Mwaka wa 2019, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kilitambuliwa kama chuo kikuu bora zaidi nchini Tanzania, hapo juu Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kilichopo mjini Morogoro.[3] UDSM kilitambuliwa kama chuo cha sitini na tisa kwa ubora zaidi wa elimu kwa Afrika.[4] Kinatambulika kama chuo cha 1885 kwa ubora wa kitaaluma duniani.[5]

Taaluma

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kinatoa programu kadhaa za shahada ya kwanza, kama vile: akiolojia, usanifu majengo, biolojia, biashara, kemia, elimu ya mawasiliano, elimu ya komputa, masomo ya maendeleo, uchumi, elimu, uhandisi na elimu ya hali ya mazingira.[6] Chuo kinatoa programu kadhaa za shahada za Uzamili na Uzamivu, kama vile: elimu ya usimamizi wa fedha, sanaa, jiografia, sheria, isimu ya lugha, fasihi, uongozi, hisabati, utabibu, muziki, lishe, fizikia, sayansi ya mimea, elimu ya siasa, saikolojia, na sanaa za maonyesho.[7]

Maisha ya Chuo Kikuu

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kina maeneo matano mjini na karibu na mji wa Dar es Salaam. Mlimani iko kilomita kumi na tatu magharibi mwa jijini.[8] Chuo Kikuu ni nyumbani kwa wanafunzi 17,098 wa shahada ya kwanza, na wanafunzi 2,552 wa shahada za uzamili na uzamivu.[9]

Watu maarufu waliohitimu Chuoni

Wahadhiri wanaofahamika

Tanbihi

  1. "Register of Universities" (PDF). Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-09-24.  Unknown parameter |[[publisher= Tanzania Commission for Universities | accessdate]]= ignored (help)
  2. 2.0 2.1 2.2 2.3 2.4 2.5 Kigezo:Cite=web
  3. "URAP - University Ranking by Academic Performance". www.urapcenter.org. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-09-25. Iliwekwa mnamo 2019-07-28. 
  4. "URAP - University Ranking by Academic Performance". www.urapcenter.org. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-09-25. Iliwekwa mnamo 2019-07-28. 
  5. "URAP - University Ranking by Academic Performance". www.urapcenter.org. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-09-25. Iliwekwa mnamo 2019-07-28. 
  6. "University of Dar es Salaam-Programme". www.udsm.ac.tz. Iliwekwa mnamo 2019-07-28. 
  7. "University of Dar es Salaam-Programme". www.udsm.ac.tz. Iliwekwa mnamo 2019-07-28. 
  8. "University of Dar es Salaam", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2019-07-20, iliwekwa mnamo 2019-07-28 
  9. "University of Dar es Salaam", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2019-07-20, iliwekwa mnamo 2019-07-28 

Viungo vya nje

Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.