Grenada
Bendera ya Grenada Nembo ya Grenada
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: Ever Conscious of God We Aspire, Build and Advance as One People
Wimbo wa taifa: Hail Grenada
Wimbo la Kifalme: God Save the King
Lokeshen ya Grenada
Mji mkuu St. George's
12°3′ N 61°45′ W
Mji mkubwa nchini St. George's
Lugha rasmi Kiingereza
Serikali

Mfalme
Gavana Mkuu
Waziri Mkuu
Ufalme wa kikatiba
Bunge kwa namna ya Westminster

Charles III
Cécile La Grenade
Keith Mitchell
Uhuru
Kutoka Uingereza

7 Februari 1974
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
344 km² (ya 203)
1.6
Idadi ya watu
 - Julai 2012 kadirio
 - Msongamano wa watu
 
109,590 (ya 185)
318.58/km² (ya 45)
Fedha East Caribbean Dollar (XCD)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC-4)
(UTC-4)
Intaneti TLD .gd
Kodi ya simu +1-473

-



Grenada ni nchi ya kisiwani kusini mwa Bahari ya Karibi. Iko kaskazini kwa Trinidad na Tobago na kusini kwa Saint Vincent.

Ni nchi mwanachama wa jumuiya ya madola na mkuu wa Dola ni Mfalme Charles III wa Uingereza anayewakilishwa kisiwani na Gavana Mkuu.

Jiografia

Eneo la nchi ni kisiwa kikuu cha Grenada pamoja na visiwa kadhaa za funguvisiwa ya Grenadini kama vile Carriacou, Petit Martinique, Rhonde Island na vingine vidogo.

Idadi kubwa ya wakazi iko Grenada penyewe pamoja na miji ya St. George's (mji mkuu), Grenville na Gouyave.

Visiwa vyote ni vya asili ya kivolkeno vyenye ardhi yenye rutuba. Grenada ina milima, na mkubwa zaidi ni mlima St. Catherine wenye kimo cha mita 840.

Watu

Wakazi ni 110,000: walio wengi (82%) ni wa asili ya Afrika wametokana na watumwa waliopelekwa huko kulima mashamba ya miwa au ni machotara (13%) waliotokana na watumwa wale na mabwana wao Wafaransa. Waliobaki (5%) ni Wazungu na Wahindi. Wananchi walio wengi wanaishi nje: ni kama mara mbili kuliko waliobaki nchini.

Lugha rasmi ni Kiingereza, lakini walio wengi kwa kawaida wanaongea Krioli.

Upande wa dini, karibu wote ni Wakristo, hasa wa Kanisa Katoliki (53%). Kati ya madhehebu ya Uprotestanti, wanaongoza Waanglikana.

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Grenada
Makala hii kuhusu maeneo ya Bahari ya Karibi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Grenada kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.