Guadeloupe | |||
| |||
Nchi | ![]() |
||
---|---|---|---|
Mji mkuu | Basse-Terre | ||
Eneo | |||
- Jumla | 1,628 km² | ||
Idadi ya wakazi (2016) | |||
- Wakazi kwa ujumla | 394,110 | ||
Tovuti: http://www.cr-guadeloupe.fr/ |
Guadeloupe ni eneo la ng'ambo na mkoa (departement) wa Ufaransa katika Bahari ya Karibi lenye visiwa tisa vidogo. Hivyo ni sehemu ya Umoja wa Ulaya.
Makao makuu ni Basse-Terre, ingawa mji mkubwa ni Pointe-à-Pitre.
Wakazi asilia walikuwa Waindio. Utamaduni wao uliharibiwa kabisa kwa kuja kwa ukoloni kutoka Ulaya (1493).
Ilikuwa koloni la Ufaransa halafu la Uingereza halafu la Uswidi halafu la Ufaransa tena.
Eneo lake ni km² 1,628.
Idadi ya wakazi ni 394,110. Asilimia 71 za wakazi ni wa asili ya Afrika au machotara. Wazee wao waliletwa huko kama watumwa kwa ajili ya kazi za mashamba ya miwa. 15% ni Wahindi, 9% Wazungu, 3% Wachina na 2% Waarabu.
Lugha rasmi ni Kifaransa, lakini wengi wanaongea pia Krioli.
Upande wa dini, 80% ni Wakatoliki na 5% Waprotestanti.
![]() |
The Wikibook Geography of France has a page on the topic of |
Angalia mengine kuhusu Guadeloupe kwenye miradi mingine ya Wikimedia: | |
![]() |
Fafanuzi za Kiingereza kutoka Wiktionary |
![]() |
picha na media kutoka Commons |
![]() |
misaada ya kujisomea kwa Kiingereza kutoka Wikiversity |
![]() |
nukuu kutoka Wikiquote |
![]() |
matini za ushuhuda na vyanzo kutoka Wikisource |
![]() |
vitabu kutoka Wikibooks |
![]() |
Makala hii kuhusu maeneo ya Bahari ya Karibi bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Guadeloupe kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |