Papa Eleutero (kwa Kigiriki Ελευθέριος) alikuwa Papa kuanzia takriban 171/177 hadi kifo chake takriban 185/193[1]. Alitokea Nikopoli, Ugiriki.
Alimfuata Papa Soter akafuatwa na Papa Viktor I.
Egesipo aliandika kwamba alikuwa shemasi wa Roma chini ya Papa Aniseti na Papa Soter.
Chini yake uzushi ulienea [2] na Eleutero aliandika kitabu kuupinga [3]
Wafiadini wa Lyon, wakiwa gerezani, walimuandikia barua nzuri sana kuhusu kudumisha amani ya Kanisa[4].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
![]() |
Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Papa Eleutero kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |