Papa Pius I alikuwa papa kuanzia takriban 142/146 hadi kifo chake takriban 157/161[1]. Alitokea Aquileia, Italia[2][3] na labda baba yake aliitwa "Rufinus".[4]. Hakika alikuwa ndugu wa Herma, aliyewahi kuwa mtumwa akawa mwandishi wa kitabu maarufu "Mchungaji"[5].
Alimfuata Papa Hyginus akafuatwa na Papa Anicetus.
Alipinga uzushi wa Gnosi hata kumtenga Marcio na Kanisa[6][7].
Chini yake, Yustino alifundisha katekesi mjini Roma na kupambana na aina mbalimbali za Gnosi [8].