Papa Stefano I alikuwa Papa kuanzia tarehe 12 Machi 254 hadi kifodini chake tarehe 2 Agosti 257[1][2]. Alitokea Roma, Italia, ingawa aliweza kuwa na asili ya Ugiriki.
Alimfuata Papa Lucius I akafuatwa na Papa Sisto II.
Alifundisha kwamba waliobatizwa na madhehebu yaliyojitenga na Kanisa Katoliki wameungana na Kristo moja kwa moja, hivyo hawahitaji wala hawatakiwi kubatizwa tena[3], tofauti na walivyodai baadhi ya maaskofu, hasa wa Afrika Kaskazini. Baadaye msimamo wake ulienea kote katika Kanisa la Kilatini.
Inasimuliwa kwamba aliuawa na maaskari wa Kaisari Valerian wakati wa Misa[4] .
![]() |
Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Papa Stefano I kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |