Papa Theodor I alikuwa Papa kuanzia tarehe 12 Oktoba/24 Novemba 642 hadi kifo chake tarehe 14 Mei 649[1]. Mzaliwa wa Yerusalemu (Israeli)[2] ambapo baba yake alipata kuwa askofu [3], alikimbilia Roma Waislamu walipoteka Nchi Takatifu[4].
Alimfuata Papa Yohane IV akafuatwa na Papa Martin I.
Alipinga uzushi wa waliokanusha Yesu kuwa na utashi wa kibinadamu na kwa ajili hiyo aliandaa Mtaguso wa Laterano wa mwaka 649 akishirikiana na Maksimo Muungamadini.
Tangu kale anaheshimiwa na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Theodorus, natione Grecus, ex patre Theodoro episcopo de civitate Hierusolima
![]() |
Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Papa Theodor I kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |