Papa Boniface I alikuwa Papa kuanzia tarehe 28/29 Desemba 418 hadi kifo chake tarehe 4 Septemba 422[1]. Alitokea Roma, Italia, alipopewa ushemasi na Papa Damaso I.
Alimfuata Papa Zosimus[2] akafuatwa na Papa Selestino I.
Kabla ya kuchaguliwa Papa alikuwa balozi wa Papa Inosenti I huko Konstantinopoli[3].
Kama Papa alijitahidi kurudisha uelewano na kudumisha nidhamu ndani ya Kanisa[4][5] na kutetea mamlaka ya Kanisa la Roma katika Iliriko[6].
Alimuunga mkono Agostino wa Hippo dhidi ya uzushi wa Upelaji[7]
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.
![]() |
Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Papa Boniface I kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |