Papa Sergio I alikuwa Papa kuanzia tarehe 15 Desemba 687 hadi kifo chake tarehe 7 Septemba 701[1]. Alitokea Syria[2] au alizaliwa Palermo (Italia) katika familia kutoka Syria[3].
Alimfuata Papa Konon[4][5][5][6][7] akafuatwa na Papa Yohane VI.
Alimfanya mmisionari Wilibrodi kuwa askofu wa Wafrisia na alimaliza farakano la Akwileia (698)[5].
Alikataa kabisa[8][9] kuthibitisha kanuni zilizotungwa na maaskofu wa Mashariki[10] katika Mtaguso wa tano-sita zikilenga kufanya desturi za Konstantinopoli zifuatwe na Wakatoliki wote[11][12]. Kwa sababu hiyo kaisari Justiniani II aliagiza akamatwe na kuletwa Konstantinopoli, lakini watu walizuia utekelezaji wa amri hiyo[5][13].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu, hasa tarehe ya kifo chake[14].
|url-access=
ignored (help)
![]() |
Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Papa Sergio I kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |