Papa Urban I alikuwa Papa kuanzia tarehe 14 Oktoba 222 hadi kifo chake tarehe 23 Mei 230[1]. Alitokea Roma, Italia.
Alimfuata Papa Kalisto I akafuatwa na Papa Ponsyano.
Urban I ni Papa wa kwanza ambaye tarehe zake zina hakika ya kihistoria[2]. Inaonekana hakukuwa na dhuluma za serikali wakati wa Upapa wake, lakini alipaswa bado kupambana na farakano la Hipoliti wa Roma[3] pamoja na kuongoza kwa uaminifu Kanisa la Roma miaka minane.
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu, hasa tarehe 19 Mei, sikukuu yake[4].
![]() |
Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Papa Urban I kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |