Papa Alexander I.

Papa Alexander I alikuwa Papa kuanzia takriban 108/109 hadi kifo chake takriban 116/119[1]. Alitokea Roma, Italia[2].

Alimfuata Papa Evaristus akafuatwa na Papa Sixtus I.

Taarifa mbalimbali zinadokeza kuwa Alexander alichangia sana ustawi wa liturujia na jimbo kwa jumla.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu, pengine mfiadini, ingawa hatajwi tena katika Martyrologium Romanum.

Sikukuu yake ni tarehe 3 Mei au 16 Machi.

Tazama pia

Tanbihi

  1. https://www.vatican.va/content/vatican/en/holy-father.index.html#holy-father
  2. http://www.santiebeati.it/dettaglio/51675

Marejeo

Viungo vya nje