Papa Sixtus I (au Xystus) alikuwa Papa kuanzia takriban 117/119 hadi kifo chake takriban 126/128[1][2]. Alitokea Roma, Italia na jina la baba yake lilikuwa Pastor[3].
Alimfuata Papa Alexander I akafuatwa na Papa Telesphorus[4].
Alishughulikia liturujia ya Kanisa la Roma [5] bila kulazimisha majimbo mengine hata kuhusu suala la adhimisho la Pasaka ya Kikristo lililoanza kujitokeza.
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu mfiadini na kutajwa katika Kanuni ya Kirumi.