Papa Celestino V, O.S.B. (1215 – 19 Mei 1296) alikuwa Papa kuanzia tarehe 5 Julai/29 Agosti 1294 hadi 13 Desemba 1294[1]. Alitokea Molise, Italia[2].
Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Pietro Angelerio wa Morrone. Baada yake hakuna tena Papa aliyejichagulia jina la Celestino.
Alimfuata Papa Nikolasi IV baada ya miaka miwili ya pengo[3], akichaguliwa kutokana na umri wake mkubwa na sifa ya utakatifu na utendaji miujiza.
Ni maarufu kwa kuwa mwaka uleule alijiuzulu[4] kwa kujitambua hawezi Upapa [5] ili arudi kuishi maisha ya upwekeni kama mmonaki (mwaka 1244 alikuwa ameanzisha shirika la Waselestini, tawi la Wabenedikto)[6]. Lakini Papa Bonifasi VIII aliyemfuata alimfunga akafuta karibu maamuzi yake yote.
Alitangazwa na Papa Klementi V kuwa mtakatifu tarehe 5 Mei 1313[7].
Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Papa Celestino V kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |